Welcome

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA KWA MARA NYINGINE TENA HUKU MKUTANO WA G20 UKIENDELEA

Makombora aina ya Scud ambayo Korea Kaskazini ililipua hivi karibuni
Jeshi la Korea Kusini linasema Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa marefu baharini saa chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kukutana na Rais wa Uchina Xi Jinping pambizoni mwa mkutano mkuu wa nchi 20 zenye zilizostawi zaidi kiuchumi duniani.Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Hwangju.

Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini Bi Park ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano zaidi na Uchina, ambayo ni mshirika wa Korea Kaskazini, kuhusu kile alichosema ni uchokozi wa mara kwa mara wa Pyongyang ambayo imekuwa ikifanya majaribio ya mabomu ya nyuklia na makombora.

Vyombo vya habari Uchina vimesema Xi amesisitiza pingamizi zake dhidi ya kujengwa kwa mfumo wa Marekani wa kujikinga dhidi ya makombora nchini Korea Kusini. Amesema mpango huo huenda ukazidisha uhasama.

WAZIRI MAHIGA KUSHIRIKI UANGALIZI WA UCHAGUZI WA WABUNGE KATIKA JAMHURI YA SHELISHELI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix Michel.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa Shelisheli, Alix Michel.

Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk. Augustine Mahiga nchini Shelisheli.


Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki)

Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 

Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8 - 10 Septemba, 2016.

Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na waangalizi kutoka nchi za SADC .

Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix Michel Rais wa Sheliseli .

Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.

Imetolewa na :
BALOZI INNOCENT E. SHIYO.

KESI YA UPINZANI KUPINGA USHINDI YATUPWA MBALI ZAMBIA


Rais Edgar Lungu wa Zambia

Mahakama ya kikatiba nchini Zambia imetupilia mbali kesi ya mgombea wa urais wa chama cha upinzani cha United Party for National Development Hakainde Hichilema na mgombea mwenza Geofrey Bwalya dhidi ya uchaguzi wa rais Edgar Lungu.Katika uamuzi wa wengi ,jopo la majaji katika mahakama hiyo ya kikatiba liliamua kwamba mda wa mwisho uliowekwa kusikiliza kesi hiyo ulikuwa umekwisha.

Bwana Lungu alihifadhi kiti chake baada ya kujipatia zaidi ya asilimia 50 ya kura katika uchaguzi huo uliofanyika tarehe 11 mwezi Agosti. Chama cha UPND cha mpinzani wake Hakainde Hichilema kilipinga matokeo hayo na kuwasilisha ombi la kuyapinga mnamo tarehe 19 mwezi Agosti.

Hakainde Hichilema wa chama cha UPND ZambiaSheria inasema kuwa mahakama ya kikatiba ina siku 14 kusikiliza kesi hiyo.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa muda huo ulikumbwa na mabishano na ilipofika siku ya Ijumaa mawakili wa bwana Hichilema waliondoka katika mahakama wakidai ukosefu wa muda. Mahakama hiyo iliendelea mapema leo na kutangaza uamuzi huo

UJUE UWANJA WA AMAAN, ZANZIBAR


Uwanja wa Amaan mjiniUnguja ni wa kihistoria, japo wengi hawafahamu. Ulijengwa kwa msaada wa serikali ya China na ulifuynguliwa mwaka 1970, ukiwa ni mradi mkubwa wa nchi hiyo wa viwanja vya michezo barani Afrika. Michezo na sherehe nyingi hufanyika uwanjani hapo. Sherehe kubwa ya kihistoria ilifanyika February 5, 1977 wakati vyama vya TANU na Afro Shirazi vilipoungana na kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM. Uwanja huo ulifungwa kwa muda na kufanyiwa ukarabati mkubwa kabla ya kufunguliwa tena mwaka 2010. Una uwezo wa kukaa watu 15,000. 
Pia ni uwanja wa kwanza kuweza kuchezewa mechi usiku hapa nchini.

DC NDEJEMBI AFANYA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA YA KONGWA NAKUBAINI UFUJAJI WA PESA


Mkuu wa wilaya ya kongwa, Mh Deogratius Ndejembi amefanya kikao cha baraza la wafanya biashara wa wilaya ya kongwa, likiwa linajumuisha wafanya biashara wote wakiwamo wafanya biashara za mazao, mifugo, na biashara zingine. 

Kikao kilifunguliwa na Mh DC akiwa kama mwenyekiti wa Baraza hilo kwa nafasi yake, Mh DC Ndejembi alipokuwa akifungua kikao alisema nakusisitiza haya, Kuwa kwa mara ya kwanza yeye kama DC anafanya kikao hicho kama Mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara hivo anaomba nakusisitiza ahitaji kuona Mtu anasimama nakuanza kulalamika hovyo, kama anamalalamiko aseme na kisha atoe utatuzi au maoni yakutatua hizo kero anazozilalamikia.


DC Ndejembi amefanya kikao hicho nakubaini kuna Posho nyingi na gharama kubwa sana ambazo zinatumika kwa Vikao vya Baraza hilo, ikiwemo gharama za Posho, Chakula, Uchapishaji wa nyaraka mbali mbali ambazo pia amezilalamikia kwakuwa kikao hicho kuna wajumbe wa kikao wamekosa Baadhi ya nyaraka za Vikao ambazo ukitizama Gharama za kikao hicho Wameorodhesha Machapisho na hayakuwapo ndani ya kikao lakini matumizi yanaonyesha pesa imetoka kwa ajili ya machapisho ya kikao.

DC Ndejembi amewaasa kuacha tabia zakuwa tegemezi kwani sasaivi wamekuwa wakizifuja pesa hizo kwakuwa ni Pesa zakupewa na LIC (Local Investment Climete) kuna siku msaada huo utakwisha hivyo, waache Tabia zakulipana posho hovyo hovyo wakati vikao wanavyofanya ni vikao vyakujadili mambo yao ya msingi kwa biashara zao na kwafaida ya Taifa lao na vizazi vyao, waanze kuchangia wao wenyewe ili wawe na uchungu na pesa zao na watajadili mambo ya msingi zaidi kwakuwa na uchungu na uzalendo zaidi.


DC Ndejembi amewaeleza wafanya biashara hao kuacha Tabia za kuweka michanga na mawe katika baadhi ya mazao ambayo yanauzwa Kongwa na hasa katika Soko kuu lakimataifa la Kibaigwa! kwani ndani ya kikao hicho kuna mjumbe alisema nakukili kulalamikiwa kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kongwa na Mkoa wa Dodoma kuwa na Tabia yakujaa mawe na michanga katika mazao ili yaongezeke kilo nakujipatia faida zaidi, kitu ambacho kinasababisha soko la mazao ya ukanda huo kushuka thamani kwa michezo hiyo michafu.


Mkuu wa wilaya kaagiza kuanzia leo Atakaebainika kachanganya Mawe au Michanga katika Mazao basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

MASHINDANO EAC YAANZA KIGALI TANZANIA YASHIKA NAFASI HII HAPA .

Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda 
Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda 
Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.
Wanarianda walioshiriki mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki wakichuana wakati wa Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo Tanzania imeshika nafasi ya Tatu.
(picha na Selemani Semunyu)

Na Seleamani Semunyu JWTZ.
MASHINDANO ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yameingia Siku yake ya kwanza baada ya kuzinduliwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu katika Riadha kwa wanawake katika mbio zilizokuwa na Ushindani Mkali na kufanyika katika Uwanja wa APRC Kicukiro. .

Mtanzania Catherine Lange aliiwezesha Timu ya JWTZ kuibuka na Ushindi wa tatu huku kwa Wanaume Mwanariadha Fabiano Nelson kufanya vyema licha kukosa ushindi wa jumla kutokana na kuwa peke yake mbele nyuma ya wakenya waliochukua ushindi wa Kwanza. 

Awali akifungua mashindano hayo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James Kabarebe amewapongeza Wakuu wa Majeshi Kutoka Nchi za Afrika Mashariki kwa kuendeleza michezo na kutoa nafasi kwa nchi zo kushiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yamekuwa kiungo katika kuimarisha Ushirikiano.

Aliyasema hayo leo wakati akizindua michezo hiyo katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Majeshi kutoka majeshi ya Nchi Nne zinazoshiriki Michuano hiyo.

“ Michezo ni Sehemu ya Majukumu ya Jeshi Lakini nawapongeza na kuyapa uzito mashindano haya kwani yamekuwa yakitusaidia katika kuimarisha ushirikiano wa Nchi hizo ili kuhakikishia inaendelea kuwa sehemu salama.

Waziri Jenerali Kabarege alitoa Wito kwa Wakuu hao kutumia nafasi ya Michezo hii kufanyia kazi changamoto kama zipo zinazokabili majeshi katika ukanda huu.

Awali Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba aliwahahakikishia Wanamichezo maandalizi Mazuri na kuwataka kuwa huru na kuchanganyika na Wanyarwanda ambao alidai wameajiandaa kuwapokea.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambaye ni Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro amesema anamatumaini makubwa kwa Timu za Tanzania kurejea na vikombe.

MTOTO ALIYEWEKEWA BETRI KWENYE MOYO KURUHUSIWA KUPITA KWENYE MAENEO HAYA BILA KUKAGULIWA.

Kadi ya kumtambulisha mtoto Happiness John (5) kimataifa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa betri ndani ya moyo inatengenezwa nchini Afrika Kusini. Happiness ambaye alifanyiwa upasuaji huo Julai 15 na kuruhusiwa kutoka hospitalini wiki moja iliyopita, anatakiwa kuwa na kadi tambulishi ambayo itamuwezesha kutofanyiwa ukaguzi wa kielektroniki. 

Kwa sasa mtoto huyo amepewa kadi ya muda ambayo inamruhusu kutopita katika maeneo yenye mionzi kwa ajili ya ukaguzi, ikiwamo viwanja vya ndege na majengo yenye ulinzi mkali.

TUNDU LISSU AIJIA JUU SEKRETARIETI YA MAADILI .


TUMECHOKA kuvumilia! Ni kauli ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kudai kusakamwa na Serikali .

Chama hicho kimetoa kauli hiyo leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya Jaji Mstaafu, Salome Kaganda ambaye ni Kamishna wa Maadili na Mtendaji Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwaandikia barua viongozi wa chama hicho akiwatuhumu “kukiuka masharti ya Hati ya Ahadi ya Uadilifu wa Viongozi wa Umma.”

Jaji Kaganda aliwaandikia barua viongozi hao tarehe 4 mwezi huu ambapo Chadema wameitaka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuacha vitisho kwa viongozi wa chama hicho.

Walioandikiwa barua hiyo ni Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema na Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.

Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, kwa mujibu wa barua ya Jaji Kaganda, katika tarehe, muda na siku ambayo haijulikani, viongozi hao wa Chadema walitoa matamshi ambayo yanachochea wananchi kutotii sheria, kufanya vurugu, kudharau misingi ya demokrasia iliyopo nchini na kutishia usalama wa nchi.

“Hata hivyo, Jaji Kaganda hakuyataja matamshi hayo wala kuyafafanua. Aidha, alidai kwamba matamshi hayo yanatokana na maazimio yaliyofikiwa na kikundi cha watu wachache nje ya Bunge,” amesema Dk. Mashinji.

Licha ya kudai kwamba, maazimio ya kikundi hicho yanapuuza utangamano, utulivu na usalama wa wananchi wengine kinyume na dhana ya maslahi mapana ya umma, Jaji Kaganda hakukitaja kikundi hicho cha watu wachache nje ya bunge huku pia akidai matamshi ya viongozi hao yalilenga ‘kushamirisha ‘ maslahi yao binafsi na maslahi ya Chadema.

“Mheshimiwa Mbowe ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama kikuu cha upinzani hapa nchini. Ni kiongozi wa chama ambacho mgombea urais wake alipata zaidi ya kura milioni sita kati ya kura 15 milioni zilizopigwa kwenye uchaguzi mkuu wa urais mwaka jana.

“Ni mbunge wa kuchaguliwa na kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Katika Bunge. Ni mtu na kiongozi anayejulikana na kuheshimika ndani na nje ya Tanzania. Kusema kuwa kiongozi huyo anaongoza kikundi cha watu wachache nje ya Bunge kwenyewe ni kuonesha maadili yenye mashaka kwa mwandishi wa barua hiyo,” amesema Dk. Mashinji.

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki ameeleza kushangazwa na barua ya Jaji Kaganda akisema;

“Ni vigumu kuamini kwamba, barua hii imeandikwa na mwanasheria na mtu ambaye amewahi kushikilia madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

“Barua ambayo haina maelezo yoyote ya kile kinachodaiwa kuwa kosa; haitaji tarehe, siku, muda au mahali kosa hilo lilipotendeka.

“Haitaji vifungu vya sheria yoyote iliyokiukwa na wala kuonyesha kama sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma ina mamlaka kisheria ya kushughulikia kosa hilo, in onyesha mapungufu makubwa ya kitaaluma na kiuandishi ya kamishna wa maadili na katika mazingira ya kawaida, ingestahili kupuuzwa,” amesema Lissu.

Kwa mujibu wa Lissu ambaye ni mwanasheria wa chama hicho, Chadema haiwezi kuipuuza barua hiyo na kwamba, inaashiria kuwepo kwa njama za kuwafungulia mashtaka katika Mahakama ya Maadili Viongozi hao ambao ni wabunge kwa lengo la kuwavua ubunge.

Aidha, mojawapo ya vigezo vya kikatiba vya mtu kukosa sifa ya kuwa mbunge ni pamoja na kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, kamishna wa maadili ana mamlaka ya kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma na kuunda mahakama (Tribunal) ya kusikiliza tuhuma hizo na kupeleka taarifa ya mashauri hayo kwa kamishna ambaye atapaswa kuwasilisha nakala za taarifa hiyo kwa rais na spika wa Bunge.

“Rais Magufuli na washauri wake wanafahamu ugumu wa kutumia mahakama za kawaida kwa lengo la kukandamiza wapinzani.

“Licha ya matatizo yake mengi, Mahakama ya Tanzania imedhihirisha mara nyingi uwezo wa kulinda uhuru wake na kutokuwa tayari kutumika kwa malengo ya kisiasa ya watawala.

“Sasa Magufuli (Rais John Magufuli) na washauri wake wanaandaa mazingira ya kuitisha Mahakama ya Kangaroo watakayoidhibiti wao ili kuhakikisha wanawakandamiza viongozi wakuu wa chama chetu.

“Kama ambavyo tumethibitisha mara kwa mara chama chetu hakitakuwa tayari kuona viongozi wake wakikandamizwa kwa kutumia kivuli cha maadili ya viongozi wa umma. Tutapambana na njama hizo. Kwa uthabiti na kwa weledi ule ule ambao tumepambana na njama nyingine za aina hiyo katika siku za nyuma,” ameeleza Lissu.

Aidha Jaji Kaganda amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo akikana kujua kuhusu barua hiyo huku akisema “mimi sifahamu kuhusu suala hilo, sina taarifa.”

RC MONGELLA ATOA UFAFANUZI KUHUSU ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MWANZA.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP.Clodwig Mtweve. 

**** Judith Ferdinand (BMG), Mwanza ****

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, leo amesema, Rais Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia kesho agosti 10 na 11, ambapo atapokelewa hiyo kesho wilayani Sengerema akitokea Chato mkoani Geita alikokuwa na mapumziko mafupi.

"Rais Magufuli atawasili kesho asubuhi katika mkoa wetu akitokea Chato mkoani Geita na ataanza ziara katika wilaya ya sengerema kwa ajili ya kuwasalimia wananchi, kuwapa taarifa za mikakati na maendeleo awamu ya tano pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi". Amesema Mongella.

Pia amesema hiyo kesho Rais Magufuli atasimama maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwasalimu wananchi kabla ya kuwasili wilayani Nyamagana.

Ametanabaisha kwamba Rais Magufuli ataitimisha ziara yake kesho kutwa agosti 11, kwa kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza, pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiasi ambapo ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo. 

Mongella amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Furahisha ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi baada ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi.

USAIN BOLT KUSTAAFU RIADHA MWAKANI

Mwanariadha Usain Bolt amedokeza kustaafu riadha ifikapo Februari mwaka 2017 baada ya michuano ya Mabingwa wa Dunia, na kuongeza kuwa hii itakuwa ni michuano yake ya mwisho ya Olimpiki kushiriki.


Mwanariadha huyo raia wa Jamaica anayeshikilia rekodi za mita 100 na 200 duniani, pia amesema anadhamiria kuwa mwanariadha kwa kwanza kukimbia kwa sekunde 19 katika mbio za mita 200.

Bolt anaweza kuondoka Rio na mafanikio ya kutwa tena medali za dhahabu tatu za mbio za mita 100, mita 200 na mbio za 4x100mita kupokezana kijiti kama ilivyokuwa mwaka 2008 na 2012.

DRAKE AFUNGUKA KUHUSU RIHANNA,


Rapa kutoka Canada, Drake alikuwa akitumbuiza katika ukumbi wa Madison Squre Garden huko New York weekend hii na kuonesha hisia zake za kumkubali Rihanna na kueleza kuwa anatamani na anaweza kuwa na mahusano na mwanadada Rihanna kama mambo yakiwa sawa.

Kabla ya kuimba nyimbo alizokuwa amepanga kuperfom usiku huo, Drake alianza kwa kusem anapata upendo wa dhati kutoka kwa Rihanna na anatamani sana kama angekuwa na mahusiano nae kwani yeye pia anamkubali sana mwanadada huyo.

“If you`ve got love for Rihanna in New York City, Cuz you know i`ve got love for Rihanna” alieleza huku akionesha tabasamu kabla ya kumkaribisha Future kuja kufungua tamasha hilo.

Riri pamoja na Drake wamekuwa wakionekana sana kwenye kumbi mbalimbali za Starehe lakini pia, wamekuwa wakileta wasiwasi zaidi hasa wanapokuwa jukwaani wakiimba nyimbo kwa pamoja na wamekuwa marafiki kwa muda mrefu sasa lakini hata siku moja hawajawahi kutangaza kuwa katika mahusiano.

Wawili hao ambao wametabiriwa kuja kuwa Couples zenye nguvu zaidi siku za usoni wamekuwa wakienda taratibu sana katika mambo yao na kuonesha dalili za kuwa na uhusiano kwani Drake aliwahi kuzungumza mbele ya mashabiki zake kuwa yupo tayari kuwa na mwanadada huyo lakini Rihanna hajawahi kuonesha lolote juu ya hilo.

Drake pamoja na Rihanna wamewahi kutamba kwa pamoja katika vibao mbalimbali kama vile ‘Take care’, ‘what`s my name’ na kibao kinachotikisa zaidi kwa sasa katika ulimwengu wa muziki ‘Work’ ambacho mwanadada Riri amemshirikisha rapa huyo.

ANIMALS - facts and info


Slow Lorises facts and info:
- Slow Lorises are primates/mammals originating from Southeast Asia.
- The Slow Loris possesses a toxic (strong venomous) bite. It is a very rare trait for a mammal indeed. The venom servers as a defence against enemy animals but also the Slow Loris mothers lick the fur of their babies to protect them (by spreading the venom).
- The adult Slow Loris weight is between 2 – 3 pounds.

- Slow Lorises have a range of habitats over a vast area of southern and south-eastern Asia.
- They are endangered due because of their habitat loss and also hunting for illegal pet and traditional medicine trades.
- Slow Lorises diet consist of mainly fruits but also insects, little reptiles, birds and bird eggs.


- In some parts of Asia the Slow Loris is well respected animal – and it is believed it can cure more than 50 diseases.
- Slow Lorises could also eat tree leaves or tree gum.
- The Slow Lorises can be found in a number of locations in Asia, including: China, Indian subcontinent, etc...

- Slow Lorises have very special pincer-like hands and feet and are perfectly adapted to live on the trees and above the ground.
- The Slow Lorises could live up to 20 years in captivity.
- Slow Loris has large eyes and is adapt at seeing in the dark providing the ability to hunt for small animals during night.


- Currently, there are five to eight species of Slow Loris recognised. The prime species are Greater Slow Loris, Pygmy Slow Loris, Javan, Benga and Bornean.
- All the Slow Loris species are listed as Endangered or Vulnerable.
- Little is known about Slow Lorises social structure. It is known though that they communicate to each other by scent marking.

- The name 'Loris' is Dutch in nature and means 'clown', which probably comes from the facial features that help to define the species.
- One of the biggest challenges for the Slow Loris is reproduction. Slow Lorises reproduce slowly, and the infants are initially put over branches or carried by either parent. 
- The slow Loris is omnivores, eating small animals, insects, fruit, vegetables, tree gum, and other vegetation.

- The sexual maturity of the Slow Loris comes after 18 months and they can start mating.
- Slow Lorises are nocturnal animals and they use scent marking to communicate with each other either for mating or threatening other animals.
- The illegal trading is really huge problem for Slow Lorises. Together with the habitat loss those are the primary reasons for declining Slow Lorises population.


- Naturally the Slow Lorises live in South-eastern Asia and Western Indonesia.
- The pygmy loris (Nycticebus pygmaeus) lives in the same area, and is similar in behaviour to the Slow Loris.
- The Slow Loris preferred habitat includes tropical forests, secondary forests and suburban gardens.

- The Slow Loris is a nocturnal primate with forward-facing eyes and human-like hands with an opposable thumb.
- Slow Lorises have a round head, large eyes (adapted at seeing at nigh), narrow snout, and a variety of distinctive coloration patterns that are species-dependent.
- The Slow Loris could be found in South and Southeast Asia. The range of countries it could be found in is: From Bangladesh to Northeast India and in the west to the Philippines in the east, and from the Yunnan province in China in the north to the island of Java in the south.

- Many previous classifications could not identify all the Slow Loris species. Now we know there are at least eight different Slow Loris species that are considered valid.
- The Slow Loris is amongst the rarest primate on our planet. The scientists consider them to be devolved specie from their closest cousins “the African bushbabies” – probably about around 40 million years ago.
- Slow Lorises sleep during the day, rolled up in a ball with their head between their legs.

- Usually the Slow Lorises are seen as slow movers but actually they frequently ’race walk’ and can move up to 8km per night. Equally the Lorises are able to remain totally still for hours on end if required.
- The Slow Loris is also closely related to the remaining lorisoids, as well as the Lemurs of Madagascar.
- The greatest cause for Slow Lorises decline is the demand for exotic pet or traditional medicine compared to the loss of their natural habitat.



- Slow Lorises have really slow pregnancy – more than 6 months to produce little babies weighting less than 50 g.
- Slow Lorises movement looks similar to the snake’s one. The twisting movement we all see is caused by having several more vertebras in their spine compared to the other primates.
- Slow Lorises arms and legs are nearly equal in length. On top of that their trunk is long, allowing them to twist and extend to nearby branches.

- In their natural habitat the Slow Lorises could live up to 25 years.
- They mate once every per 1 – 1.5 years.
- The Slow Loris’s grasp is very strong allowing the animal to freeze in their current position for hours as they stalk their prey.

- Slow Lorises have a toxic bite – and should not be pets! It is actually the only lorisid primate that is venomous.
- The Slow Loris moves slowly and makes very little noise so when threatened it can freeze and almost become invisible.
- Their second finger is reduced for gripping. Also the Slow Lorises have the longest tongues of all the primates (compared to body size). They use the tongue to drink water or nectar.


- The Slow Loris venom can kill and there is currently no known cure. Although scientifically not clear how they evolved the poison – the reason for the venom is primarily defence.
- Slow Lorises often use their both hands to eat while hanging upside-down from branches using their feet.
- The Slow Lorises are protected from International commercial trade and many laws. Despite all the efforts though the animals are still sold openly at many Asian markets and illegally imported into many countries.

- The evolutionary history of the Slow Lorises is uncertain as the fossil records are scarce and the molecular clock studies provided inconsistent results.
- Slow Lorises have many enemies. Sadly the biggest treat is the man. The other predators hunting for Lorises are hawks, eagles, snakes, orangutans, and even cats, civets and bears.
- The hands and feet of Slow Lorises adapted very well to allow them hold and grasp branches for very long periods of time.

- Slow Lorises males are highly territorial and very competitive towards other males.
- Although the Slow Loris is a small mammal, their home ranges can be huge – sometimes even the size of 35 football pitches.
- The Slow Loris toxin is produced by licking a gland on their arm, and the secretion mixes with its saliva to become active.

- Slow Lorises number of young is 1 to 2 offspring every 1 – 1.5 years
- Slow Lorises are very popular as pets in some You Tube channels 
- The Slow Lorises are solitary nocturnal animals that sleep through the day and hunt during the night.

- Sadly, many Slow Lorises have their teeth removed for the purpose of pet trade. Many Lorises die from blood loss, infections, poor nutrition or poor handling.
- The pregnancy period of a female Slow Loris is about 190 days.
- Sadly there are very deep beliefs about the supernatural powers of the Slow Lorises. They are considered to protect from evil spirits or cure wounds and conditions. Many animals are killed for the purpose of the traditional medicine.

amazing new Top 10 Animal Fight HOT VIDEO INSIDE

THIS IS TERRIBLE SEE VIDEO INSIDE Last Feast of The Crocodiles VS chimpanzee

Second snakes that lay eggs , so why the Cobra roadster .see this war

© Copyright LECTURE SKILLS
Back To Top