Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakiingia Uwanjani wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Baadhi ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda.
Wanarianda walioshiriki mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki wakichuana wakati wa Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo Tanzania imeshika nafasi ya Tatu.
(picha na Selemani Semunyu)
Na Seleamani Semunyu JWTZ.
MASHINDANO ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yameingia Siku yake ya kwanza baada ya kuzinduliwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu katika Riadha kwa wanawake katika mbio zilizokuwa na Ushindani Mkali na kufanyika katika Uwanja wa APRC Kicukiro. .
Mtanzania Catherine Lange aliiwezesha Timu ya JWTZ kuibuka na Ushindi wa tatu huku kwa Wanaume Mwanariadha Fabiano Nelson kufanya vyema licha kukosa ushindi wa jumla kutokana na kuwa peke yake mbele nyuma ya wakenya waliochukua ushindi wa Kwanza.
Awali akifungua mashindano hayo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James Kabarebe amewapongeza Wakuu wa Majeshi Kutoka Nchi za Afrika Mashariki kwa kuendeleza michezo na kutoa nafasi kwa nchi zo kushiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yamekuwa kiungo katika kuimarisha Ushirikiano.
Aliyasema hayo leo wakati akizindua michezo hiyo katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Majeshi kutoka majeshi ya Nchi Nne zinazoshiriki Michuano hiyo.
“ Michezo ni Sehemu ya Majukumu ya Jeshi Lakini nawapongeza na kuyapa uzito mashindano haya kwani yamekuwa yakitusaidia katika kuimarisha ushirikiano wa Nchi hizo ili kuhakikishia inaendelea kuwa sehemu salama.
Waziri Jenerali Kabarege alitoa Wito kwa Wakuu hao kutumia nafasi ya Michezo hii kufanyia kazi changamoto kama zipo zinazokabili majeshi katika ukanda huu.
Awali Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba aliwahahakikishia Wanamichezo maandalizi Mazuri na kuwataka kuwa huru na kuchanganyika na Wanyarwanda ambao alidai wameajiandaa kuwapokea.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambaye ni Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro amesema anamatumaini makubwa kwa Timu za Tanzania kurejea na vikombe.
_____________________________________
“How long are you going to wait before you demand the best for yourself and in no instance bypass the discriminations of reason? You have been given the principles that you ought to endorse, and you have endorsed them. What kind of teacher, then, are you still waiting for in order to refer your self-improvement to him? You are no longer a boy, but a full-grown man. If you are careless and lazy now and keep putting things off and always deferring the day after which you will attend to yourself, you will not notice that you are making no progress, but you will live and die as someone quite ordinary.
From now on, then, resolve to live as a grown-up who is making progress, and make whatever you think best a law that you never set aside. And whenever you encounter anything that is difficult or pleasurable, or highly or lowly regarded, remember that the contest is now: you are at the Olympic Games, you cannot wait any longer, and that your progress is wrecked or preserved by a single day and a single event. That is how Socrates fulfilled himself by attending to nothing except reason in everything he encountered. And you, although you are not yet a Socrates, should live as someone who at least wants to be a Socrates.”
― Epictetus
Post a Comment