Mkuu wa wilaya ya kongwa, Mh Deogratius Ndejembi amefanya kikao cha baraza la wafanya biashara wa wilaya ya kongwa, likiwa linajumuisha wafanya biashara wote wakiwamo wafanya biashara za mazao, mifugo, na biashara zingine.
Kikao kilifunguliwa na Mh DC akiwa kama mwenyekiti wa Baraza hilo kwa nafasi yake, Mh DC Ndejembi alipokuwa akifungua kikao alisema nakusisitiza haya, Kuwa kwa mara ya kwanza yeye kama DC anafanya kikao hicho kama Mwenyekiti wa Baraza la wafanyabiashara hivo anaomba nakusisitiza ahitaji kuona Mtu anasimama nakuanza kulalamika hovyo, kama anamalalamiko aseme na kisha atoe utatuzi au maoni yakutatua hizo kero anazozilalamikia.
DC Ndejembi amefanya kikao hicho nakubaini kuna Posho nyingi na gharama kubwa sana ambazo zinatumika kwa Vikao vya Baraza hilo, ikiwemo gharama za Posho, Chakula, Uchapishaji wa nyaraka mbali mbali ambazo pia amezilalamikia kwakuwa kikao hicho kuna wajumbe wa kikao wamekosa Baadhi ya nyaraka za Vikao ambazo ukitizama Gharama za kikao hicho Wameorodhesha Machapisho na hayakuwapo ndani ya kikao lakini matumizi yanaonyesha pesa imetoka kwa ajili ya machapisho ya kikao.
DC Ndejembi amewaasa kuacha tabia zakuwa tegemezi kwani sasaivi wamekuwa wakizifuja pesa hizo kwakuwa ni Pesa zakupewa na LIC (Local Investment Climete) kuna siku msaada huo utakwisha hivyo, waache Tabia zakulipana posho hovyo hovyo wakati vikao wanavyofanya ni vikao vyakujadili mambo yao ya msingi kwa biashara zao na kwafaida ya Taifa lao na vizazi vyao, waanze kuchangia wao wenyewe ili wawe na uchungu na pesa zao na watajadili mambo ya msingi zaidi kwakuwa na uchungu na uzalendo zaidi.
DC Ndejembi amewaeleza wafanya biashara hao kuacha Tabia za kuweka michanga na mawe katika baadhi ya mazao ambayo yanauzwa Kongwa na hasa katika Soko kuu lakimataifa la Kibaigwa! kwani ndani ya kikao hicho kuna mjumbe alisema nakukili kulalamikiwa kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kongwa na Mkoa wa Dodoma kuwa na Tabia yakujaa mawe na michanga katika mazao ili yaongezeke kilo nakujipatia faida zaidi, kitu ambacho kinasababisha soko la mazao ya ukanda huo kushuka thamani kwa michezo hiyo michafu.
Mkuu wa wilaya kaagiza kuanzia leo Atakaebainika kachanganya Mawe au Michanga katika Mazao basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
_____________________________________
“How long are you going to wait before you demand the best for yourself and in no instance bypass the discriminations of reason? You have been given the principles that you ought to endorse, and you have endorsed them. What kind of teacher, then, are you still waiting for in order to refer your self-improvement to him? You are no longer a boy, but a full-grown man. If you are careless and lazy now and keep putting things off and always deferring the day after which you will attend to yourself, you will not notice that you are making no progress, but you will live and die as someone quite ordinary.
From now on, then, resolve to live as a grown-up who is making progress, and make whatever you think best a law that you never set aside. And whenever you encounter anything that is difficult or pleasurable, or highly or lowly regarded, remember that the contest is now: you are at the Olympic Games, you cannot wait any longer, and that your progress is wrecked or preserved by a single day and a single event. That is how Socrates fulfilled himself by attending to nothing except reason in everything he encountered. And you, although you are not yet a Socrates, should live as someone who at least wants to be a Socrates.”
― Epictetus
Post a Comment