Welcome

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAZIRI MAHIGA KUSHIRIKI UANGALIZI WA UCHAGUZI WA WABUNGE KATIKA JAMHURI YA SHELISHELI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Shelisheli, Alix Michel.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akimtambulisha Balozi Innocent Shiyo kwa Rais wa Shelisheli, Alix Michel.

Rais wa Shelisheli, Alix Michel akiwa kwenye kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Baloz Dk. Augustine Mahiga nchini Shelisheli.


Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki)

Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Organ), katika Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. 

Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8 - 10 Septemba, 2016.

Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa chaguzi za kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga (Mb), alizindua rasmi misheni hiyo tarehe 2 Septemba, 2016 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya waangalizi itakua na waangalizi kutoka nchi za SADC .

Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix Michel Rais wa Sheliseli .

Pia Mheshimia Waziri Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Seychels.

Imetolewa na :
BALOZI INNOCENT E. SHIYO.

_____________________________________

“How long are you going to wait before you demand the best for yourself and in no instance bypass the discriminations of reason? You have been given the principles that you ought to endorse, and you have endorsed them. What kind of teacher, then, are you still waiting for in order to refer your self-improvement to him? You are no longer a boy, but a full-grown man. If you are careless and lazy now and keep putting things off and always deferring the day after which you will attend to yourself, you will not notice that you are making no progress, but you will live and die as someone quite ordinary.

From now on, then, resolve to live as a grown-up who is making progress, and make whatever you think best a law that you never set aside. And whenever you encounter anything that is difficult or pleasurable, or highly or lowly regarded, remember that the contest is now: you are at the Olympic Games, you cannot wait any longer, and that your progress is wrecked or preserved by a single day and a single event. That is how Socrates fulfilled himself by attending to nothing except reason in everything he encountered. And you, although you are not yet a Socrates, should live as someone who at least wants to be a Socrates.” ― Epictetus

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright LECTURE SKILLS
Back To Top